Posts

Showing posts with the label Tanzanian News

Kwanini Afrika inamlilia Fidel Castro

Image
Mwalimu Nyerere akiwa na Fedel Castro wakati wa uhai wao. Na LEAH H. MWAINYEKULE, DESEMBA 10, 2013 wakati dunia nzima ikiwa inafuatilia matangazo ya moja kwa moja ya kumbukumbu ya kifo cha Rais Nelson Mandela, jambo la kihistoria lilifanyika:  Rais Barack Obama wa Marekani alishikana mkono na Rais Raul Castro wa Cuba.  Wakati huo huo, Seneta Ted Cruz wa Marekani, alitoka nje wakati Raul Castro aliposimama kutoa hotuba kwenye tukio hilo. Rais Obama alikuwa Rais wa pili wa Marekani kuushika mkono wa kiongozi wa Cuba, katika kipindi cha miaka 60.  Mwaka 2000, Rais Bill Clinton alishikana mikono na kaka wa Raul ambaye alikuwa kiongozi wa Cuba wakati huo, Rais Fidel Castro.  Hilo lilitokea wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa huko New York na Wamarekani wengi walitoa shutuma kutokana na mkono huo. Tukio la Rais Obama kusalimiana kwa mkono na Raul Castro, liliripotiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi....

SALAMU ZA LEMA ZATUA MKUTANO WA MAJALIWA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Arusha jana, wakati alipowasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuhutubia mkutano wa hadhara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Na ELIYA MBONEA-ARUSHA  MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Secilia Pareso (Chadema), amewasilisha salamu za Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, katika mkutano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. Pareso alimtaja Lema aliyefutiwa maombi yake ya dhamana juzi na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha katika ziara ya Majaliwa mkoani hapa tangu jana, ilikuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, kuomba viongozi waliokuwa meza kuu kusalimia wananchi kwa dakika tatu tu. Mkutano huo wa Majaliwa ulifanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa jana. Pareso aliyesimama baada ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Catherine Magige, kusailimia wananchi, alianza kwa kushukuru kwa Majaliwa kufika na kutembelea Arusha na alisisitiza kuwa maendele...

LOWASSA: MIKUTANO YA NDANI MITAMU

Image
Edward Lowassa Na JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema anamshukuru  Rais Dk. John Magufuli kwa kuruhusu vikao vya ndani. Amesema vikao hivo,  “ni vitamu zaidi kuliko vile ya nje.” Hayo aliyasema   Dar es Salaam alipofungua mafunzo ya siku mbili kwa madiwani, wabunge na viongozi wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam yanayoendelea kutolewa na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la   Ujerumani. Akizungumzia   ziara za kanda zilizofanywa na viongozi wa chama hicho  hivi karibuni, Lowassa alisema vikao vya ndani vimewapa nafasi na muda mwingi wa kuzungumza na wanachama  kwa karibu zaidi. “Tumefanya ziara, tumeona hali ya barabara ni nzuri lakini hali ni nzuri zaidi tulivyozungumza na wanachama wetu na tunamshukuru Rais. “Aliona hakuna haja ya mikutano ya nje akatupatia vikao vya ndani, Loh! Ni vizuri, ni vitamu zaidi k...